LAKINI KUNA MKANGANYIKO MTAMBUKA AMBAO WATU WENGI WAMEKUWA NA DHANA MBALIMBALI JUU YA NDOA, SWALI JE!? NDOA NI NINI?
Ni muungano wa Mwanaume na Mwanamke unakubarika kidini na kiutamaduni ambao na unatarajiwa kudumu kuwapa haki sawa za kijinsia na kutosheleza majukumu mengine ya kijamii
Waebrania 13:4
4 Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.
Moja kati ya mambo makuu saba matakatifu ambayo MUNGU aliyaanzisha baada ya uumbaji ni NDOA
BAADA YA UUMBAJI WA VIUMBE VYOTE ADAMU ALIPEWA JUKUMU LA KUWAPA MAJINA kama inavyoeleza hapo chini.
Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
habari hii itaendelea....... sehemu ya pili usikose kunifuatilia maana ndoa ni shida na chanzo cha mumonyoko wa maadili katika familiya zetu.