Kutoka juu ya kilele cha mlima wa mizeituni, Yesu aliutazama mji wa
Yerusalemu. Hekalu lile maarufu lilionekana wazi. Jua la jioni lilitupa miale
yake myeupe ya kuta za mawe na marumaru ing'aayo tangu mnara wake wa dhahabu
mpaka chini. Mwisraeli ye yote angewezaje kulitazama bila kusifu kwa jinsi
iliyvokuwa maarufu! Lakini Yesu alikuwa na mawazo mengine “Alipofika karibu
aliuona mji, akaulilia” Luka 19:41.
Machozi ya Yesu hayakuwa kujililia mweneywe, ingawa mbele yake palikuwa
na Getsemane, mahali pa mateso makali yaliomkabili, na Kalwari, mahali pa
kusulubishwa pake. Walakini siyo
mambo hayo yaliyomtia huzuni kiasi cha kulia. Aliwalilia maelfu ambao
watafikwa na ajali waliomo Yerusalemu.
Historia ya miaka elfu ya watu wa Mungu walio wateule, na jinsi Mungu
alivyokuwa akiwaangalia kwa huruma nyingi, ilipita katika macho yake
Yerusalemu, mji uliotukuzwa na Mungu kuliko yote duniani mwote. “Bwana
ameichagua Sayuni …… akae ndani yake”. Zab. 132:13. Kwa muda wa vizazi vingi
manabii watakatifu walikuwa wakitoa ujumbe wa maonyo. Damu za kondoo zilikuwa
zikitolewa kila siku kafara zikielekeza kwa Mwanakondoo wa Mungu.
Kama Israeli angedumisha ushirika wake na mbingu, Yerusalemu ungedumu
milele, maana ni mteule wa Mungu. Lakini historia nzima ya watu hawa walipendwa
na Mungu imekuwa ya uasi tu. Mungu alikuwa amewahurumia watu wake zaidi ya
upendo wa Baba kwa mtoto wake. “Kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao
yake” 2Mambo ya Nyakati 36:15. Maonyo na kusihi kote viliposhindwa, aliwatumia
kipaji maarufu kabisa cha mbinguni, mwana wa Mungu mwenyewe, ili kushughulikia
mji muasi. Kwa muda wa miaka mitatu Bwana na Nuru na utukufu, amekuwa akienda
huku na huko kati ya watu wake, “Akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa
na Ibilisi”. “Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona
tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka uliokubaliwa”. “Vipofu
wanapata kuona, viwete wanatembea wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia,
wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema” Matendo 10:38; Luka
4:18; Mathayo 11:5.
Aliishi kati yao bila kuwa na makao maalumu ili apate kuwasaidia katika
hali zao za kuhurumiwa, akiwasihi ili wapate kukikubali kipawa cha mbinguni,
ambacho ni cha uzima. Huruma zake nyingi zilikataliwa na waasi hawa kwa
masikitiko makubwa. Lakini Israeli alimkataa rafiki yake mkuu na msaidizi wake
wa pekee. Kusihi kwake kwa upendo mwingi kumedharauliwa na kukataliwa.
Muda wa rehema na msamaha ulikuwa unatoweka. Mkusanyo wa ghadabu kwa
ajili ya uasi wao, ambao ni wa muda mrefu, ulikuwa umejaa karibu kupasuka juu
yao. Yule ambaye ndiye angeweza kuwaokoa na ajali dhahiri iliyokuwa
ikiwakabili, amedharauliwa, amekataliwa na karibu atasulubishwa.
Kristo alipoutazama Yerusalemu na ajali yake ikiukabili, pamoja na
taifa zima, aliona maangamizo yake yote kwa ukamilifu. Alimwona Malaika mwenye
upanga tayari kuharibu na kuangamiza mji ambao umekuwa makao ya Mungu kwa muda
mrefu. Kutokea mahali pale pale alipokuwa akisimama mpaka sehemu yote ya mji
ambao baadaye Titus jemadari alisimama pamoja na jeshi lake, alitazama ng'ambo
pale hekalu takatifu liliposimama. Machozi yakilengalenga machoni mwake, akiona
jinsi kuta za mji zitakavyozungukwa na majeshi ya wageni. Alisikia vishindo vya
majeshi vikijipanga kwa vita. Alisikia sauti za akina mama na watoto wao
wakililia chakula, wakati mji umezingirwa na majeshi ya adui. Aliona nyumba
takatifu ya Mungu ikiteketea katika ndimi za moto, na maangamizo makuu.
Akitazama mbele katika vizazi vingi aliona watu wa agano na Mungu
wakitawanyika katika nchi zote, kama “mavunjiko jangwani”. Huruma za Mungu,
upendo usio kifani, unaonekana katika maneno ya maombolezo ya Yesu juu yao. “Ee
Yerusalemu, Yerusalemu, uuaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa
kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wake, kama vile kuku
avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa yake, lakini hamkutaka”
Mathayo 23:37.
Kristo aliona katika Yerusalemu mfano wa ulimwengu ambao ni mgumu kwa
kutokuamini na uasi, nao una haraka kuingia katika hukumu za Mungu. Roho yake
ilijaa huzuni kwa ajili ya maangamizo ya nchi. Alitamani kuwaokoa wote. Alikuwa
tayari kujitoa kabisa mpaka kifo ili kuwaletea watu wote wokovu.
Mtukufu wa mbinguni analia! Jambo hilo laonesha jinsi ilivyo kazi ngumu
mno ya kumwokoa mkosaji na matokeo ya kuvunja sheria ya Mungu. Yesu aliuona
ulimwengu umehusika katika uasi sawa na Yerusalemu ulivyoangamizwa kwa uasi ule
ule.
Dhambi kuu ya Wayahudi ilikuwa ile ya kumkataa Kristo. Dhambi kuu ya
ulimwengu ni ile ya kukataa sheria ya Mungu, ambayo ndio msingi wa utawala
wake, mbinguni na duniani. Watu mamilioni waliomo dhambini ambao wataangamia,
katika mauti ya pili watakataa kusikia ukweli katika wakati wao wa wokovu.
UJUMBE HUU UANALETWA KWENU NA CHARLES SHIBITA PUNDA WA YESU .
hapa hakuna maele.zo ya mkato yesu anakuja upesi sana tuache dhambi.
KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NUMBER 0763371047 au pshibita@gmail.com