Naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu;
na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu akisema, umeanguka,
umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa masikani ya mashetani, na ngome ya kila roho
mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza …. Nikasikia sauti
nyingine kutoka mbinguni, ikisema, tokeni kwake enyi watu wangu, msishiriki
dhambi zake, wala msipokee mapigo yake” Ufunuo 18:1-2,4.
Tangazo lililotolewa na malaika wa pili wa ufunuo 14:8 linarudiwa tena
hapa pamoja na nyongeza ya adhabu inayomhusu Babeli, tangu tangazo la kwanza lilipotolewa
.
Hapa inaelezwa hali ya kutisha sana. Kwa kukataa ukweli, mioyo ya watu
itazidi kuwa giza zaidi na zaidi nao watazidi kushupaa. Wataendelea kukanyaga
mojawapo ya amri za Mungu, mpaka watafikia hatua ya kuwatesa, wale wanaoitunza
amri hiyo. Kristo atadharauliwa pamoja na Neno Lake na watu wake.
Jina la dini litakuwa kama vazi la kufunika maovu, yaani watu watajidai
kuwa dini, lakini sivyo. Kule kuamini pepo kwamba ni maongezi na wafu,
kunafungulia mafundisho ya shetani, na kuingiza mivuto ya malaika waovu iwe
kanisani. Babeli imejaza kikombe cha ghadhabu ya uovu wake, na uangamivu wake
uko karibu kutokea.
Lakini Mungu bado anao watu wake katika Babeli, na watu waaminifu hawa
lazima watolewe humo, ili wasishiriki dhambi zake na wasipate mapigo yake
malaika anashuka kutoka mbinguni aking'arisha nchi kwa utukufu wake, na kutaja
maovu ya Babeli. Wito unasikika, “Tokeni kwake enyi watu wangu”. Wito huu ndio
maonyo ya Mungu ya mwisho kwa ulimwengu.
Uwezo wote wa ulimwengu ukijiuna pamoja ili kupingana na sheria ya
Mungu, utatangaza wazi kuwa “watu wote, wadogo kwa wakubwa, matajiri kwa
maskini, walio huru na watumwa” (Ufunuo 13:16) lazima wafuate mpango wa kanisa,
na kupumzika katika sabato ya uongo (Jumapili). Watakaokataa kufuata amri hiyo
mwishoni watatajwa kuwa wanastahili kuuwa. Kwa upande mwingine sheria ya Mungu
inayohusiana na pumziko la Mwumbaji, yaani siku ya sabato, inatishia adhabu
kubwa kwa wale watakaoivunja.
Tukiwa na jambo linalotangazwa wazi namna hii, mtu yeyote
atakayeikanyaga siku ya Mungu, yaani sabato ya siku ya saba, na kutii siku
iliyoamriwa na binadamu, atapokea alama ya mnyama na sanamu yake, alama ya
uwezo wa kibinadamu, mtu kama huyo huwa amechagua kumtii mtu badala ya Mungu.
“Mtu yeyote akimsujudia huyo myama na sanamu yake, na kuipokea chapa
katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika
mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji,
katika kikombe cha hasira yake, naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika
watakatifu, na mbele za Mwana Kondoo”. Ufunu 14:9-10.
Hakuna mtu atakayestahili kuteswa mateso hayo mpaka awe amepata ukweli
sawasawa na akaukataa. Wengi hawajapata nafasi ya kusikia ujumbe maalum,
unaopasa kwa wakati huu Mungu aonaye mioyo yote hawezi kumwacha mtu yeyote
anayehitaji maonyo haya. Kila mtu atapata nafasi ya kufanya uamuzi wake kwa
hakika.