Ndipo ukaja
utukufu wa uungu katika mapenzi ya Babaye, Akasema, “Lakini ni kwa ajili ya
hayo nilivyoifikia saa hii. Baba, ulitukuze jina lako.” Ni kwa kifo cha Kristo
tu, ndio utawala wa Shetani ungeangushwa, mwanadamu akombolewe na Mungu
atukuzwe.
Yesu
aliikubali dhabihu, akakubali kuteseka kama Mchukua Dhambi.
Sauti
ikatoka ndani ya wingu liliotanda juu ya kichwa chake; “Nimelitukuza nami
nitalitukuza tena.” Katika mateso ya kiungu kibinadamu yajayo Kristo,
atalitukuza jina la Baba yake.
Sauti
iliposikika nuru ilimzunguka Kristo, kana kwamba mkono wa nguvu za Uungu
uliomzungushia ukuta wa moto.
Hakuna mtu
aliyethubutu kusema kitu. Wote walisimama wakimwangalia Yesu. Ushuhuda wa Baba
ukiwa umetolewa, wingu liliinuka na kutawanyika hewani.
Wayunani
waliokuwa wamekuja kumwulizia waliliona wimgu, wakaelewa maana yake na
kumtambua
Kristo,
hakika; kwao alidhihirishwa kama Aliyetumwa na Mungu. Sauti ya Mungu ilikuwa
imesikika wakati wa Ubatizo wa Yesu, na wakati Yesu alipogeuka sura mlimani.
Sasa kwa
mara ya tatu ilisikika katika kundi la watu wengi. Yesu alikuwa ametoa wito
wake mara ya mwisho, na kutamka maafa yatakayowapata Wayahudi.
Na sasa Mungu anamtambua yule aliyekataliwa na
Israeli.
Yesu
akasema: “Sauti hiyo haikuwako kwa ajili, yangu, bali kwa ajili yenu. ” Ilikuwa
ni ushuhuda kutoka kwa Mungu kwamba Yesu alikuwa amesema ukweli, na kwamba yeye
ni Mwana wa Mungu.
“Sasa hukumu
ya ulimwengu huu ipo; sasa,” Kristo aliendelea kusema, “mkuu wa ulimwengu huu
atatupwa nje,” “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. Aliyanena
hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa”. Ikiwa mtakuwa kipatanisho kwa
dhambi za wanadamu, ulimwengu utaangazwa.
Uwezo wa Shetani kuwashikilia watu utavunjika.
Sura ya Mungu iliyoharibiwa itarudishwa kwa wanadamu, na jamii ya wenye haki
waaminio watayarithi makao ya mbinguni.
Mwokozi
aliuona msalaba, jinsi ulivyo wa ukatili na aibu yake pamoja taabu zake,
ukiwaka kwa utukufu. Lakini ukombozi wa mwanadamu si yote yaliyomalizwa na
msalaba.
Upendo wa Mungu unadhihirishwa ulimwenguni.
Doa lililotiwa mbinguni na Shetani linaondolewa kwa milele. Malaika na watu
watavutwa kwa Kristo. “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,” Alisema “nitawavuta wote
kwangu.”
Watu wengi
walikuwa wamemzunguka Kristo alipokuwa akisema maneno haya; “Walakini ajapokuwa
amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini.”
Ishara
zisizohesabika zilikuwa zimetolewa lakini watu walifumba macho yao na kufanya
mioyo migumu. Kwa vile sasa Baba mwenyewe alikuwa amenena na hawakuwa na la
zaidi kuuliza, bado walikataa kuamini.
“Walakini
hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya
Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi”.
Katika
kujikinga na fedheha na aibu walimkana Kristo na kukataa toleo la uzima wa
milele. Ole kwa wale, ambao hawakutambua wakati wao uliowajilia! Taratibu na
kwa huzuni Kristo aliondoka hekaluni milele.