MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

SIRI MAFANIKIO MWAKA 2018.


Mjue sana MUNGU,ili uwe na amani.Ndivyo mema yatakavyokujia"-Ayubu 22:21


Image result for kombe la dunia 1998


1 wathesalonike 5:17 “Ombeni bila kukoma.



Maombi ni njia ambayo wanadamu tunawasiliana na Mungu wetu. Kama ambavyo tunawasiliana na ndugu zetu, marafiki, wazazi, wachumba wetu kila mara na kila wakati ndivyo Mungu wetu anatamani tuongee nae daima. Kwa hiyo maombi ni kuufungua moyo kwa Mungu kana kwamba kwa rafiki, tukizifungua siri za moyo wetu kwake. Mungu anatamani tumweleze furaha yetu, huzuni  zetu, dhambi zetu na yale yanayotusumbua tuyaweke kwake katika wasaa wa maombi apate kututimizia kama Baba yetu. Kwa mantiki hiyo maombi sio kumjulisha BWANA kitu kipya au asichokijua la hasha! anajua yote ila tunapaswa kuonyesha uhitaji wetu kwa kumweleza yale yaliyoko moyoni bila unafiki wowote au kuficha neno lolote. Watu wengi wamekuwa wakiogopa kumwendea Mungu kwa sababu wanahisi hawezi kuwasikia hivyo wanakata tamaa lakini huo ni uongo wa ibilisi. Leo tutaangalia mambo machache kuhusu maombi nakusihi uzidi kumwomba Mungu akusaidie ili uweze kuelewa zaidi maana elimu kuhusu maombi ni pana sana.


Image result for MJUE SANA MUNGU
AHADI 6 ZA BWANA YESU KUHUSU MAOMBI
1. Mathayo 18:19,20
“Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”
Nampenda Bwana Yesu. Yani kila tukutanikapo wanadamu wawili huwa si wawili tena bali tupo watatu. Maana Bwana Yesu hujihudhurisha kuja kuchukua maombi yetu ampe Baba.
2. Marko 11:22-24
“Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”
3. Yoh. 14:13,14 ‘Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya’
Msisitizo: – Bwana Yesu anasema lolote tutakaloomba!
4. Yoh. 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. ”
Kukaa ndani ya Kristo na maneno yake kukaa ndani yetu huo ni ushirika katika mahusiano yetu na Mungu. Ni ushirika wa kudumu. Ushirika wa kila siku. Ni ushirika ambao ulianzishwa pale msalabani na Kristo mwenyewe. Damu yake ilipomwagika pale msalabani kwa ajili ya kutusafisha dhambi zetu, ilianzisha mahusiano yasiyo na kikomo. Kumuamini Bwana Yesu na kumkiri kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu ni mwanzo wa mahusiano hayo ya kudumu katika Kristo. Kuokoka ni hatua ya mwanzo. Na tunapaswa kuendelea na mahusiano na Kristo kwa Roho Mtakatifu.
5. Yoh. 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni”
6. Yoh 16:23,24 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. - Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. -”
Hakuna masharti ya NINI TUOMBE ila kuna masharti ya NAMNA YA KUOMBA:
i. Kupitia jina la Yesu
ii. Mtu aombaye awe na mahusiano na Mungu
iii. Mwombaji awe na Imani
Ubarikiwe sana.


Subscribe to receive free email updates: