MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

KWANINI YESU NI MUNGU? KWA MJIBU WA BIBLIA

UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU


Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu Kristo ni Mungu.Ikiwa sisi ni wanafunzi wa Biblia tusiwe kama wengine wanaosema kuwa Yesu si Mungu.Kama huna moyo wa jiwe  kama  wengine waliotiwa upofu kiroho na kushindwa kuyaelewa maandiko,Je,unaamini kuwa Yesu ni Mungu?  Yesu ni Mungu na ushahidi mwingi wa maandiko upo.


KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA MAANDIKO

Image result for yesu ni mungu mkuu


Hapa tunaona maandiko yakimtaja Yesu KriNasto waziwazi kuwa ni Mungu. Katika  ( 1YOHANA. 5:20 )“Nasi twajua kuwa Mwana wa Mungu amekwisha kuja,naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli.,yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo.Huyu ndiye MUNGU WA KWELI NAUZIMA WA MILELE”.. Pia katika ( YOHANA 20:26-29 ) “basi,baada ya siku nane,wanafunzi wake walikuwamo ndani tena,na Tomaso pamoja nao.Akaja Yesu na milango ilikuwa imefungwa,akasimama katikati,akasema,Amani iwe kwenu.Kisha akamwambia Tomasolete hapa kidole chako;uitazame mikono yangu;ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu;wala usiwe asiyeamini;bali aaminiye.Tomaso akajibu akamwambia,BWANA WANGU NA MUNGWANGU..Yesu akamwambia,wewe kwa kuwa umeniona umesadiki;wa heri wale wasioona wakasadiki”.YESU KRISTO MUNGU MKUU, ( 1TITO 2:13  )  “Tukilitazamia tumaini lenye mafunuo ya KRISTO YESU MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU”.. YESU NI MUNGU aliyejifunua katika mwili ( WARUMI 9:5 )  “Na katika hao alitoka KRISTO KWA NJIA YA MWILI,NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE,MUNGU,MWENYE KUHIMIDIWA MILELE.AMINA..Mhalifu msalabani alimwita YESU Mungu na kumuomba YESU atakapokuwa katika ufalme wake amkumbuke mharifu huyo”. ( LUKA 23:39-43 ).Yesu hakukataa kuwa SI MUNGU bali alisema,Amini nakuambia leo hivi,utakuwa pamoja nami peponi.YESU NI MUNGU ALIYEKUJA DUNIANI .( WAFILIPI 2:5-6  )  “Ambaye yeye mwanzo alikuwan yuna namna ya Mungu,naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho,bali alijifanya kuwa hana utukufu,akatwaa namna ya mtumwa,akawa ana mfano wa wanadamu”.YESU alijita-mbulisha kwao kuwa ni MUNGUlakini hawakuelewa ( YOHANA 10:30-33 )  “Yesu akawajibu,kazi njema nyingi niwewaonyesha zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu,kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe;bali kwa kukufuru,na kwasababu wewe uliye.mwanadamu wajifanya kuwa Mungu. Wayahudi walisema anakufuru kwa kusema kuwa yeye ni Mungu.Kimsingi Yesu ndiye Baba mwenyewe ndio maana anasema huwezi kumtenganisha na Baba; ukimwona yeye umemuona Baba. ( YOHANA 14:7-9 )
Katika mstari 8 na 9  Filipo akamwambia,Bwana,utuonyeshe Baba yatutosha. Yesu akamwambia,Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote,wewe usinijue,Filipo?

    Ikiwa tu wanafunzi wa Yesu hatupaswi kubabaishwa na watu ambao hawana Roho wa Mungu.Mtuambaye hana Roho wa Mungu hawezi kusema Yesu ni Mungu..Kwasababu hiyo,wanatumia akili tu.Hawa ni watu wa tabia ya asili ambao hawawezi kuyaelewa  mambo ya kiroho ( 1WAKORITHO 2:14 ) “Basi,mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kuyapokea mambo ya Roho wa Mungu;maana kwake ni upuuzi;wala hawezi kuyafahamu;kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni”

YESU NI MUUMBAJI
Image result for YESU AKIWA MBINGUNI
Image result for god is the creator of the universe
Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake ( YOHANA 1:3,14 )  “vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili;nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli”.Yesu aitwa Neno la Mungu(UFUNUO 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(YOHANA 1:1)..  na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (WAKOLOSAI 1:13-16)vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani.Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.

.YESU ALIKUWEPO KABLA YA VITU VYOTE KUWEPO DUNIANI.

Image result for god is the creator of the universe


( WAKOLOSAI 1:17 ) “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote;na vitu vyote hushikamana katika yeye”.( MIKA 5:2 ) Basi,wewe Bethlehemu,Efrata,uliyemdogo kuwa miongoni mwa maelfu za Yuda;kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale;tangu milele“.

Image result for YESU AKIWA MBINGUNI


Yesu Kristo alikuwako kabla ya Nabii Ibrahimu kuwako(YOHANA 8:52-58)Watu walioambiwa maneno hayo n a Yesu mwenyewe wliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwa anakufuru.Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho,( YOHANA 4:24)..YOHANA 17:5,24.WAEBRANIA 7:3 ). Imasema  “hana baba,hana nana,hana wazazi,hana mwanzo wa siku zake,wala mwisho wa uhai wake,bali amefananishwa na Mwana wa Mungu;huyo adumu kuhani milele”.YESU ni alfa na omega ,wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (UFUNUO 22:13).Bali kwa damu ya thamani,kama ya mwana-kondoo asiye na ila,asiye na waa,yaani ya Kristo.Naye amejulikana kweli tangu zamani,kabla haijawekwa misingi ya  dunia,lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yetu ( 1PETRO 1:19-20 )
YESU NI MTAWALA JUU YA YOTE.  HII NI SIFA YA MUNGU PEKEE

 (YOHANA 330 ) “Yeye ajaye kutoka juu,huyo yu juu ya vyote.Yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia,naye anena mambo ya duniani,yeye ajaye kutoka mbinguni yuu juu  ya yote” . ( YOHANA 13:13 ) “Ninyi mwaniita ,Mwalimu, na Bwana;nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo“. ( WARUMI 14:9 ) “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii,awamiliki waliokufa na walio hai pia”. Neno kumiliki ni kutawala sifa ya kutawala ni sifa ya Mungu pekee



Image result for YESU AKIWA MBINGUNIImage result for YESU AKIWA MBINGUNI



4,YESU KRISTO NI ZAIDI YA MTU YEYOTE AU NABI AU MTUME YEYOTE YULE..

 WAEBRANIA 3:1-7 ) Mustari 3 unasema,Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahiliutukufu zaidi kuliko Musa,kama vile yeye atengenezayenyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”..Anayezungumziwa hapa ni Yesu Kristo Mungu muumbaji. YESU ,ameketi mkono wa kuume wa ukuu huko mbinguni (WAEBRANIA 1;3-4).

YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WALIMWENGU (WATU) WOTE.


( ZABURI 58:11 ), ‘Hakika yuko Mungu anayetawala katika dunia“. (UFUNUO 18;8 ) “Kwasababu hiyo,mapigo yake yatakuja katika siku moja,mauti na huzuni na njaanaye atateketeza kabisa kwa moto.Kwamaana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“.Tene ndiye atakaye ihukumu Dunia yote “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote,bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.( MATHAYO 25:31-32 ) “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake,na malaika watakatifu wote pamoja naye,ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake,naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi” .( MATENDO 10:42 ) “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( WARUMI 2:16 )  “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na injili yangu,kwa Kristo Yesu.( 2TIMOTHEO 4:1 ) “Nakuagiza mmbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu,atakayewahukumu waliohai na waliokufa;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.

YESU HABADILIKI TENE HANA KIGEUGEU.

     {WAEBRANIA 13:8} “Yesu Kristo ni yeye yule jana na leohata milele“. ( WAEBRANIA 1:10-12 ) “Wewe ,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi.Na mbingu ni kazi ya mikono yako;Hizo zitaharibika,lakini wewe unadumu;Nazo zote zinachakaa kama nguo,Na kama mavazi,utazizinga,nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,na miaka yako haitakoma“. ( MALAKI 3:6 ) Kwa kuwa mimi,Bwana,sina kigeugeu” ( ZABURI 102:26-27 ) “Hizi zitaharibika,bali wewe utadumu;Naam,hizi zitachakaa kama nguo;na kama mavazi utazibadirisha,nazo zitabadilika.Lakini wewe U yeye yule;na miaka yako haitakoma“. ( YAKOBO 1:17 ) “Kwake hakuna kubadilika,wala kivulu cha kugeukageuka”.

YESU YUPO KILA MAHALI ,KOTEKOTE DUNIANI

( MATHAYO 18:20 ) “Kwa kuwa walipo wawili watatu,wamekusanyika kwa jina langu,mimi nipo papo hapo katikati yao”. Mwenye uwezo wa kukaa mahali pote ni Mungu.



  1. YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI(MUNGU PAMOJA NA WANADAMU).

 Image result for jesus judgement day 1:23-25 ) Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”.Tabia ya Yesu inaonyesha kuwa kama mwanadamu,kuzaliwa kwake kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Hapa tunaona jinsi alivyo na uwezo wa tofauti na wanadamu akiwa anafahamu mambo yote kabla akiwa duniani..Yeye pia ajua yote yaliyomo ndani ya moyo wa mwanadamu (YOHANA 6:64,YOHANA 13:1,YOHANA 13:11,YOHANA 18:4,YOHANA 19:28).Tena Yesu alitabiri kabla jambo kutokea,pia alijitabiria mwenyewe yatakayomtokea mbele (MARKO 8:31,LUKA 9:22,LUKA 12:50,LUKA 22:37,LIKA 24:7-26,YOHANA 3:14,YOHANA 10:17-18,YOHANA 7:33,YOHANA 13:33,YOHANA 14:28,YOHANA 17:11,YOHANA 16:5,10,16,18 ).
Yesu aliabudiwa na kusujudiwa akiwa hapa duniani,Sifa ya kuabudiwa na kusujudiwa ni ya Mungu pekee hivyo Yesu ni Mungu.(MATHAYO 4:10).
  • Hata malaika wote wanamsujudia Yesu (UFUNUO 22:8-9,WAEBRANIA 1;6).
  • Ndiyo maana Yesu alisujudiwa akiwa mtoto mchanga alipozaliwa (MATHAYO 2:11,MATHAYO 14:33<LUKA 24;52).
  • Hata pepo wachafu walimsujudia Yesu (MARKO 5:2,6)


ENDELEENI NKUBARIKIWA .



Subscribe to receive free email updates: