MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

ITAMBUE HISTORIA YA DUNIA KUPITIA BIBLIA TAKATIFU

Miongoni mwa mahala ambapo wanahistoria wanakutana uso kwa uso na wanabibilia na kukukubaliana ni katika historia ya dunia kama ilivyoelezewa katika Biblia kitabu cha Daniel 2.


ili kuweka kumbukumbu sawa, Katika historia ya ulimwengu Hakuna utawala utakao dumu milele isipokuwa
ule uliotabiliwa katika kitabu cha daniel 

"...Nao utasimama milele na milele" Daniel 2:44


Kwa kujua au kutokujua Chama tawala kinawaaminisha watu wake kuwa kitadumu milele. Napenda kuwakumbusha watanzania kuwa kumewahi kuwepo Tawala Kubwa tena walitawala dunia nzima ya wakti wao lakni hawakudumu.

Tawala hizi zilizotawala dunia nzima ni kama zinavyoonekana katika sanamu hii.[​IMG]

NINI KILITOKEA

Nebukadneza akiwa mfalme wa kwanza kutawala utawala wake utadumu milele Mungu akamuonyesha kupitia ndoto kuwa hicho kitu hakitakuwepo. Wakiwa wakisherekea na kubweteka wakidhani watadumu milele walivamiwa na majeshi ya Umedi na Uajemi chini ya mtu ambaye Mungu alimtaja jina lake hata kabla hajazaliwa (Isaiah 45:1) na kuuteka mji wa babeli (kilometer 40 kutoka  katika mji wa Bagdad ya sasa iraq) na kutawala dunia. Na baadae wakabadilishana wafalme kama kwenye picha hapo juu
.

SIRI YA HISTORIA NA MWISHO WA DUNIA MUNGU ANAIFUNUA TENA KATIKA  DANIEL 7
Image result for the book of daniel and revelation

www.teuvokopra.fi



Ujumbe wa Kitabu cha Danieli - sura ya 7.

Wanyama wakubwa wanne.
1. Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.
2. Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.
3. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.
4. Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
5. Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
6. Kisha nikatazama, na kumbe! mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
7. Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
8. Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang�olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
9. Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
10. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.
11. Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.
12. Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang�anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.
13. Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
14. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
15. Basi, mimi Danieli, roho yangu ilihuzunika mwilini mwangu, na hayo maono ya kichwa changu yakanifadhaisha.
16. Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo hayo.
17. Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.
18. Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.
19. Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;
20. na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.
21. Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda;
22. hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.
23. Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.
24. Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
25. Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
26. Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuyapoteza na kuyaangamiza, hata milele.
27. Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
28. Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu. 
(DAN 7:1-28)
Sura hii ina mambo mengi.
Lakini tutachukua baadhi ya mambo muhimu.
Danieli aliona maono hayo katika mwanzo wa utawala wa Belshaza yaani hivi mwaka wa mia tano hamsini kabla ya Kristo. (550 K.K.)
Wakati huo Danieli alikuwa na miaka sabini.
Namna nyingine ya Mungu kufanya kazi ni kuwapa watu maono juu ya mambo fulani.
Tunakumbuka namna gani Farao wa Misri alivyoona maono:
Yalikuwapo masuke saba yaliyokaushwa na saba mema.
Aliamka akaona ndoto nyingine.
Walikuwapo ng�ombe saba walionona na saba waliokonda.
Yusufu alitafsiri ndoto ya Farao na kusema kwamba kwa sababu ndoto ilirudia maana yake ni kuwa, Mungu lazima amelithibitisha jambo hilo. (MWA 41:32)
Tulisoma katika Kitabu cha Danieli sura ya pili kuhusu ndoto ya Nebukadreza ya sanamu kubwa.
Sasa Mungu alimpa Danieli ndoto hiyo kuhusu mambo hayo kwa zaidi ya miaka hamsini baada ya ndoto aliyoiona Nebukadreza.
Ndoto hii ilikuwa juu ya majitu yaani wanyama wanne wakubwa.
Ndoto hizi mbili zina maana moja.
Ndoto katika sura ya pili na sura ya saba.
Hii ina maana kwamba Mungu alikuwa ameamua kwa hakika mambo hayo.
Ndoto juu ya wanyama wakubwa wanne imeandikwa katika Danieli sura ya saba mstari wa pili hadi wa kumi na nne.
Halafu Danieli anaomba ufafanuzi wa ndoto hizi katika mstari wa kumi na tano na wa kumi na sita.
Malaika anamfafanulia maana ya hizo ndoto katika mstari wa kumi na saba hadi wa ishirini na saba.
Sasa tuanze kuchunguza ndoto na maana yake juu ya wanyama wakubwa wanne.
MNYAMA WA KWANZA alikuwa SIMBA
Mstari wa nne:
4. Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu. (DAN 7:4)
Maelezo juu ya wanyama watatu wa kwanza ni mafupi sana.
Hayo yameandikwa katika mstari wa kumi na saba.
Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani. (DAN 7:17)
Wanyama wakubwa hawa ni wafalme wanne yaani falme za dunia.
Wakati wa Danieli, Babeli ilitawala dunia nzima na ilikuwa ufalme mkubwa zaidi duniani.
Pia ilikuwa ndiye Mnyama wa kwanza yaani simba.
Majengo ya Babeli yalifunikwa na mchanga baada ya miaka maelfu kupita.
Sikuhizi yanafukuliwa tena kutoka kwenye mchanga.
Wachunguzi wanapenda kuchunguza historia na kuyafuatilia mambo hayo.
Wakati wa ufukuzi wa Babeli sanamu za simba zilizoochongwa kwenye jiwe wamepatikana.
Simba ni ishara ya Babeli.
Ishara au mnyama wa ishara wa Tanzania ni twiga.
Si ajabu kwa Babeli kulinganishwa na simba katika ndoto ya Danieli.
Babeli ilitawala dunia hivi tangu miaka ya mia sita na tano hadi mia tano thelathini na tisa kabla ya Kristo. (605-539 K.K.)
Tulisoma huyu simba alikuwa na mabawa ya tai.
Ina maana kwamba mfalme wa Babeli Nebukadreza alikuwa mwindaji wa haraka na mtekaji aliyeteka dunia ya wakati ule.
Halafu tunaelezwa kwamba yule simba aling�olewa yale mabawa na kupata moyo wa mwanadamu.
Inatukumbusha ugonjwa wa akili wa Nebukadreza na maisha yaliyofuatia akimshukuru Mungu.
Hayo tulisoma katika sura ya nne.
Mnyama wa kwanza alikuwa simba na ni ufalme Babeli wa dunia nzima.
MNYAMA WA PILI alikuwa DUBU
Tulisoma katika mstari wa tano:
Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele. (DAN 7:5)
Baada ya Babeli ufalme mkubwa zaidi duniani ulikuwa Umedi-Uajemi.
Kuanzishwa kwake tulisoma katika sura ya tano.
Umedi-Uajemi ilitawala dunia baada ya Babeli tangu mwaka wa mia tano thelathini na tisa hadi wa mia tatu thelathini kabla ya Kristo. (539-330)
Huo ulikuwa utawala wa pamoja ya Waamedi na Waajemi.
Mstari wa tano unaeleza kwamba dubu aliinuliwa upande mmoja.
Mfano kwamba baadaye walizungumzia tu Uajemi yaani Irani na si kuhusu Umedi na Uajemi.
Huyo dubu alihimizwa ale nyama tele yaani afanye mapinduzi makubwa apindue dunia nzima.
Historia inaeleza kwamba sehemu hii ya ndoto ya Danieli ilitokea.
MNYAMA WA TATU alikuwa CHUI
Tulisoma katika mstari wa sita:
Kisha nikatazama, na kumbe! mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka. (DAN 7:6)
Ufalme mkubwa wa Uajemi ulimalizika wakati wa Iskanderia Mkuu, yaani Alexander Mkuu alipofanikisha kuteka Uajemi katika mwaka wa mia tatu thelathini na tatu na wa mia tatu thelathini na moja kabla ya Kristo.
Iskanderia Mkuu alikuwa mtawala wa Ugiriki yaani Uyunani.
Hivyo Ugiriki ikatawala ulimwengu tangu mwaka wa mia tatu thelathini hadi wa sitini na tatu kabla ya Kristo.
Tulisoma katika mstari wa sita kwamba mnyama wa tatu: kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege;
Mabawa ya ndege ni mfano wa ukasi yaani mbio.
Anaenda kama kwa kupaa.
Kwa miaka michache Iskanderia aliteka dunia nzima iliyojulikana ya wakati ule.
Tulisoma pia katika mstari wa sita: mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne;
Iskanderia alikuwa na wakuu wa jeshi wanne.
Kupitia hawa wakuu wanne wa majeshi alifanikiwa katika safari zake za kivita.
Iskanderia Mkuu alikufa akiwa na miaka zaidi ya thelathini kwa malaria na kudhoofishwa na pombe.
Tulisoma pia katika unabii wa Danieli kwamba mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne.
Mabawa manne ya ndege na vichwa vinne ni mfano wa wakuu wa jeshi la Iskanderia.
Alexander alipokufa ufalme wake uligawanyika sehemu nne.
Wakuu wa jeshi waligawana ufalme.
Vitabu vya historia vinaeleza juu yao na majina yao ni:
Gassander, aliyetawala Makedonia.
Lysimakus alichukua sehemu ya Trakia na sehemu ya Asia ndogo.
Ptolemaios alipata Misri.
Tutakaposoma sura ya kumi na moja tutakutana na Ptolemaios tena.
Seleukus alichukua Siria na Mashairi ya Kati.
Waliomfuatia Iskanderia hawakupata ufalme bali watoto wake na mkewe waliuawa.
Pole pole Ugiriki ilianza kukosa nguvu na Rumi ilipata nguvu.
Ilitokea kama tulivyosoma katika maono ya Danieli.
Wakati wa huo ufalme wa mnyama wa tatu ulipoisha ulianza ufalme wa mnyama wa nne.
MNYAMA WA NNE MNYAMA WA KUTISHAImage result for kitabu cha daniel 7

Tulisoma katika mstari wa saba kuhusu mnyama wa nne:
Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi. (DAN 7:7)
Danieli alitoa unabii hivyo.
Hatuelezwi kwamba mnyama wa nne anafanana na nani.
Tunaambiwa tu alikuwa mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi.
Alikuwa wa kutisha kiasi ambacho alikuwa hana mfano miongoni mwa wanyama ndiyo maana hailinganishwi na wanyama wowote.
Baada ya Ugiriki Rumi ilikuwa utawala mpya duniani.
Kwa sababu ya vita vya ndani ikagawanyika baada ya miaka mia tatu - mia nne baada ya Kristo.
Ikawa mashariki na magharibi.
Mgawanyiko ulikuwa wa kisiasa na wenye vita.
Baada ya hapo hapojatokea na utawala mpya wa dunia.
Siku hizi tunaishi katika mabaki ya utawala huo.
Tusome tena mstari wa nane.
8. Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang�olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu. (DAN 7:8)
Tulisoma katika mstari wa saba:
... naye alikuwa na pembe kumi. (DAN 7:7b)
Na tulisoma katika mstari wa nane:
... pembe nyingine ikazuka kati yao,
... mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang� olewa kabisa.
Utawala wa Rumi uko Ulaya.
Muungano wa serikali za Ulaya utaanza.
Siku hizi mambo yanazidi kuelekea huko.
Tusome tena mstari wa kumi na tisa na wa ishirini.
19. Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; 20. na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake. (DAN 7:19,20)
Danieli alitaka kupata uhakika wa pembe kumi za yule mnyama na ile iliyochipuka baadaye.
Danieli alitoa unabii, kwamba mnyama wa nne ni ufalme wa nne, yaani ufalme wa Rumi.
Hayo yalianza kabla ya Yesu, ukagawanyika sehemu mbili na baadaye sehemu nyingi baada ya miaka mamia baada ya Yesu.
Hivyo baada ya hapo hakuna ufalme wa kufanana naye.
Nchi nyingine zimejaribu kutawala ulimwengu lakini kitabu cha Danieli kinatabiri kwamba hakuna nchi itakayoweza wala kufanya hivyo.
Kwa mfano Ujerumani ilijaribu wakati wa vita vya mwisho kutawala dunia nzima.
Miaka sitini hivi iliopita.
Uingereza imetawala sehemu kubwa ya Afrika lakini haijatawala dunia nzima.
Urusi imejaribu kwa kusaidiwa na ukomunisti kuwa mtawala wa dunia nzima.
Tusome tena mstari wa ishirini na tatu hadi wa ishirini na tano.
23. Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. 24. Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu. 25. Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. (DAN 7:23-25)
Huyu mnyama alikuwa na pembe kumi yaani nchi nyingi zimeungana.
Halafu alikuwa na pembe moja ndogo.
Naelewa: hii pembe ni Mpinga Kristo.
Mambo machache yanaongelewa kuhusu pembe hii yaani Mpinga Kristo.
Aliangusha pembe tatu.
Inawezekana kwamba katika utawala wa Mpinga Kristo nchi tatu hazitakubali utawala wa Mpinga Kristo hivyo zitaondolewa.
Ilisemwa Mpinga Kristo alikuwa na kinywa kinenacho upotovu.
Ufunuo sura ya kumi na tatu inaeleza mwanzo wa Mpinga Kristo.
Alipata nguvu yake kutoka Shetani ndiyo maana anatamba.
Ilikuwa tofauti na pembe zingine yaani wafalme na watawala wengine.
Alipigana na watakatifu na aliwashinda.
Watakatifu wa nani?
Kurudi kwa Yesu kutatokea kama miaka mitatu au minne kabla ya Mpinga Kristo atapata utawala wote.
Unyakuo umekuwa mahubiri yenye nguvu hivyo wengi watageuka na kutubu dhambi zao na wataokoka.
Wakati huo wataishi wa mwisho wa kanisa la Laodikia.
Ni wakati wa wanawali watano wajinga waliorudi kutoka kununua mafuta.
Mwanzo wa ghadhabu Wakristo watakuwa na amani.
Uamsho utaenea kwa nguvu.
Hapo Mpinga Kristo atapata utawala na mateso yataanza.
Tulisoma kwamba anasema maneno ya kumpinga Aliyejuu yaani anamdhihaki Mungu.
Tulisoma pia kwamba pembe moja ilifanya vita na watakatifu ikawashinda.
Ni dhihaka yenye nguvu.
Hapo watatumia televisheni, redio na magazeti yote.
Hayo yanaelekea kwenye mateso na Wakristo wengi watauawa.
Tulisoma pia kwamba Mpinga Kristo atabadili nyakati na sheria.
Hayo yatapewa kwake kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Siku hizi duniani kuna njia mbali mbali za kuhesabu miaka.
Nyingi zimehesabiwa tangu kuzaliwa kwa Kristo.
Yaani hesabu za miaka zinazungumzia Yesu.
Hayo yanamchokoza Mpinga Kristo.
Hivyo ataunganisha hesabu za nchi mbali mbali ili aweze kutawala dunia nzima vizuri.
Na pia atavuruga hesabu za nyakati kwa sababu watu wanahesabu kutoka katika Biblia urefu wa ghadhabu.
Mpinga Kristo atabadili sheria kuwa ngumu kwa Wayahudi na Wakristo.
Tulisoma kwamba nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati, yaani kwa miaka mitatu na nusu.
Mambo haya yanapatikana katika Ufunuo pia.
Hiyo inaeleza juu ya utatu wa kazi ya Mpinga Kristo.
Kwanza: - Wakati - una maana ya mwaka moja yaani kuingia katika utawala kwa Mpinga Kristo.
Pili: - Nyakati mbili - yaani miaka miwili.
Ni muda wa kazi za Mpinga Kristo.
Mwisho: - Nusu wakati - yaani nusu mwaka, ambayo ni kuvamia kwa Mpinga Kristo juu ya Israeli na mambo ya mwisho wa ghadhabu.
Halafu tusome mstari wa tisa na wa kumi.
9. Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa. (DAN 7:9,10)
Anayezungumziwa hapa ni Mungu.
Hatusomi, lakini Biblia inasema katika kitabu cha Ufunuo sura ya tano mstari wa kumi na moja kwamba malaika walikuwapo milioni mia moja na moja.
Pia Danieli alitabiri katika mstari wa kumi.
.. maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake;
Malaika walikuwa milioni mia moja na moja.
Tuendelee kusoma mstari wa kumi na moja na wa kumi na mbili.
11. Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. 12. Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang�anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira. (DAN 7:11,12)
Tunaelezwa kuhusu mwisho wa ghadhabu inayoelezwa pia katika Ufunuo sura ya kumi na tisa.
MPINGA KRISTO ANAFUNGWA.
Baada ya hapo Yesu ataanzisha ufalme wa amani wa miaka elfu hapa duniani.
Tusome kuhusu hayo katika mstari wa kumi na tatu na wa kumi na nne.
13. Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. (DAN 7:13,14)
MARUDIO
Marudio mafupi juu ya wanyama wanne.
Wakati wa Danieli mambo yalikuwa unabii.
Aliangalia mbele.
Sasa tunaweza kuangalia mambo mengi nyuma.
Mnyama wa kwanza alifanana na simba na ni mfano wa ufalme wa Babeli utawala wa dunia nzima.
Mnyama wa pili aliyefanana na dubu alikuwa ni mfano wa Umedi-Uajemi na baadaye iliitwa Uajemi tu.
Uajemi ilitawala dunia baada ya Babeli.
Siku hizi Uajemi inaitwa Irani.
Mnyama wa tatu ni ufalme wa dunia yaani Ugiriki.
Ugiriki ni sawa na Uyunani.
Biblia inatumia jina: Uyunani.
Chui alikuwa mfano wa Ugiriki.
Halafu mnyama wa nne mwenye kutisha, mwenye nguvu, na mbaya.
Ulikuwa mfano wa ufalme wa Rumi wa kidunia.
Hapo ndipo Mpinga Kristo alitokea kutoka ufalme huo atakayetawala miaka mitatu na nusu.
Atajaribu kuwa kama Yesu Kristo, aliyefanya kazi miaka mitatu na nusu.
Baada ya wakati wa Mpinga Kristo Yesu ataanzisha utawala wa amani duniani.
Kwanza itakuwa hapa duniani kwa miaka elfu na baadaye milele katika umilele.
Mstari wa mwisho unasema hivi:
Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu. (DAN 7:28)
HALI YA SASA DUNIANI:
Ulimwengu unaelekea kwenye mambo hayo.
Lakini utawala wa mambo hayo hauponyoki katika mikono ya Mungu.
Tunaweza kusema: "Baba yangu anashughulikia kazi hizi za utawala, hakuna taabu!"
HABARI HII ITAENDELEA........................
 LAIKINI UJUMBE WA MUNGU NI HUUImage result for kitabu cha daniel 7

 Kisha nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu wote waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote, watu wa lugha zote na rangi zote.Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari na chemchemi za maji.” UFUNUO 14:6-7
Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.  UFNUO 1:7
Image result for the book of daniel and revelation





Subscribe to receive free email updates: