MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA
IJUE AMRI YA SABATO KATIKA BIBLIA NA ASLI YAKE

Ongeza kichwa
ASILI YA SABATO,  MWAZILISHI NI MUNGU MWENYEWE MWANZO 2:1-4 
Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. 
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 
Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu
 na nchi zilipoumbwa.


 MTOAJI WA AMRI  HII YA SABATO NI MUNGU MWENYWE
UTHIBITISHO HUU UNAPATIKANA KATIKA KITABU CHA KUTOKA 20:
zilipoumbwa.




  8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9   Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10   lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11  Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
SABATO NI UTAMBULISHO NA ISHARA KWA  WATU KUMTAMBUA MUNGU
Uthibitisho huu unapatikna katika katika kitabu cha nabii Ezekiel 20:20
20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 21 Lakini watoto hao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu, wala hawakuzishika hukumu zangu kuzitenda, ambazo mwanadamu ataishi kwazo kama akizitenda; walizitia unajisi sabato zangu, ndipo nikasema, kwamba nitamwaga ghadhabu 
SABATO NI KWA WANADAMU WOTE NA SIYO  ISRAEL TU SOMA  ISAYA 66  :22-23
22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu
 mbele zangu, asema Bwana.
KUMBUKA AMRI KUMI ZA MUNGU  IKIWEMO NA SABATO NDO MSINGI WA UPENDO WA MUNGU NA HUKUMU YAKE KWA WANADAMU WOTE SIKU YA MWISHO
Soma mhubiri inasema 12:13-14
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
ufunuo 14:12 inasema
 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. 
ufunuo12:17 inasema
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
KUMBKA YESU ANAKUJA UPESI

MBARIKIWE SANA SOMO HILI  LITAENDELEA.

Subscribe to receive free email updates: