MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

AMINI USIAMINI HIVI NDIVO ILIVOTOKEA

Watu 5 Waliofukiwa na Kifusi Kwa Siku 41 Katika Machimbo ya Dhahabu Nyangarata Waokolewa Wakiwa Hai.





WACHIMBAJI wadogo wa madini waliopotea kwa kufunikwa na kifusi kwenye mgodi wa Nyangarata, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 5 mwaka wamepatikana, watano wakiwa hai na mmoja akiwa amefariki.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Afisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wachimbaji hao ambapo amesema kuwa waliishi chini ya mgodi huo kwa muda wa siku 41 wakila magome ya miti na maji yanoyotelemka kwa nadra.

Masoud amesema kuwa wachimbaji walikuwa sita ambapo watano waliokolewa wakiwa hai baada ya kusikika na wachimbaji wa mgodi wa jirani na mgodi huo wakiomba msaada kwa ishara ya kugonga kuta za mgodi huo ndipo walipo watambua na kuitwa msaada ambapo mmoja kati ya hao alifariki dunia na kushindwa kutolewa katika mgodi huo.

Akitaja majina ya wahanga hao ni Muhangwa Amosi, Joseph Bulule, Chacha Wambula, Unjiwa Aindo, Msafiri Gerald na aliyefariki ni Mussa Supana.

Mosoud amesema kuwa wachimbaji hao watano walionusurika kufa wamelazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Kahama na hali zao bado sio nzuri ambapo amesema kuwa wizara itaendelea kutoa taarifa zaidi za wahanga hao.

Wizara ya Nishati na Madini wamewata wachimbaji wadogo watumie mfumo na dhana bora za uchimbaji wa madini ili kujihakikishia usalama wao.


Subscribe to receive free email updates: