Unapokaribishwa Ufilipino na hii massage ya Chatu mtu wangu!
Nyoka wanaofanya hii wako wanne, wamepewa majina kabisa, wanaitwa Michelle,Walter, EJ na Daniel.
Wakati ilipoanzishwa ilikuwa ni huduma ya bure, lakini kwa sasa ni biashara, chatu hao wanahitaji kula kuku kumi kila mmoja kabla ya zoezi la massage kuanza.
Msimamizi wa bustani ya wanyama ambapo inatolewa huduma hiyo, Giovanni Romarateamesema wakati wanaanza biashara hiyo wageni walikuwa wanaogopa, lakini wengi waliojaribu waliipenda na sasa hutolewa kwa kulipia, kila kinachopatikana kinatumika kuboresha bustani hiyo.