MJUE SANA MUNGU,ILI UWE NA AMANI, NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUIJIA

GENERAL NEWS Ninayo taarifa kutoka jeshi la polisi kuhusu mauaji ya Afisa Polisi Dar es Salaam…..




.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar esa salaam imetangaza kuwakamatwa majambazi sugu sita walioshiriki katika mauaji ya ASP Elibariki Pallangyo huko nyumbani kwake Temeke tarehe 04.08.2015.


Watu sita wanashikiliiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuuwa afisa wa jeshi la polisi mkoa wa morogoro ASP Elibariki Palangyo ambaye alikuwa mkuu wa kikosi cha kupambana na uhalifu hasa ujambazi wa kutumia silaha kule Morogoro‘ – Kova
Afisa huyo alikuja Dar es Salaam kuiona familia yake lakini usiku wa tarehe 4 mwezi wa nane alivamiwa na majambazi 6 nyumbani kwake Temeke na kuuliwa mbele ya familia yake , tukiwa kama jeshi la polisi tuliweza kufanya upelelezi na tumefanikiwa kuwakamata wahutumiwa wanaohusika na tukio hilo‘- Kova
‘Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita wanaohusika na tukio hilo la kumuuwa afisa huyo wakati wa kuhojiwa watuhumiwa hao walikiri kuwa ni kweli walihusika na tukio hilo la kumuuwa afisa polisi wa mkoa wa Morogoro‘ – Kova
Waliokamatwa ni: 1) OMARY SALEHE@BONGE MZITO (39) Mkazi wa Mtoni mtongani ambaye ni Kiongozi wa kundi hilo
2) SAIDI SAIDI MAZINGE (37) Mkazi wa Tegeta Kibaoni
3) RASHIDIWATSONB@ DODO(21) MKAZI WA Vingunguti
4)RAMADHANI SALUM@NGUZO 38 mkazi MBAGALLA KIBURUGWA
5) BAKARI SALIM RASHIDI@ MALENDA (38) Mkazi wa Mbagala kizuiani
6) HAMISI HAMISI @ FREEMASON 24 Mkazi wa Mbezi Mwisho
Aidha mtuhumiwa  namba mmoja alikutwa na silaha bastola aina ya revolver iliyofutwa namba na baada ya mahojiano. aidha mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu kabla ya kufariki alijaribu kuwatoraka askari kwa kukimbia alijeruhiwa na hatimaye alifia njiani wakati akipelekwa hosptalini. Pia inasemekana marehemu alipotezana na familia yake miaka mitani iliyopita akiwa kwenye harakati ya ujambazi.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayoukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, InstagramnaYouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB,

Subscribe to receive free email updates: